More details

Development Programs & Advocacy

CCT imeshiriki katika uzinduzi wa Jengo la Kituo Jumuishi cha utoaji wa huduma kwa manusura wa vitendo vya ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto lililokarabatiwa na USAID Afya yangu Northern. Jengo hili limezinduliwa rasmi na mhe. Rosemary Staki Senyamule , Mkuu wa Mkoa wa Dodoma leo Tar 27/1/2022. Mkoa wa Dodoma ni mojawapo ya Mikoa yenye vitendo vya ukatili wa kijinsia na dhidi ya watoto. Kituo hiki kitarahisisha upatikanaji wa huduma za haraka kwa waliofanyiwa vitendo vya ukatili.Kituo hiki kinapatikana katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma (General Hospital)